KARIBU BONGO CORNER ENTERTAINMENT GROUP

Karibu katika site yako iliyo bora na inayokuletea habari mbalimbali zinazoigusa dunia katika nyanja ya burudani zaidi. Kaa mkao wa kuburudika zaidi ndani ya Bongo Corner!!! More

Friday, October 24, 2014

FISI AZUA KIZAAZAA MJINI SINGIDA

Leo katika mji wa Singida eneo lifaamikalo kama sokoni aliibuka fisi na kuzua mtafaruku. Fisi huyo ambaye baada ya watu kumzonga aliingia katika moja ya duka lililokuwa wazi. Wananchi waliokuwapo eneo hilo walifanikiwa kumpiga fisi huyo na hatimaye kumuua kabisa.
Ila chaajabu watu wengi wamekuwa wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina kwani ni ajabu fisi kutokea katikati ya mji ambapo hamna ata mbuga karibu.

Thursday, October 23, 2014

WAZILI MKUU MIZENGO PINDA NAYE AFUNGUKA KUHUSU KUGOMBEA URAISI

Siyo tetesi tena. Sasa ni rasmi
kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye
amekuwa akitajwa kuwania urais
amethibitisha wazi kuwa atagombea kiti
hicho katika uchaguzi mkuu mwakani.
Alitoa uthibitisho huo juzi akiwa London,
Uingereza ambako yuko katika shughuli za
kikazi. Hatua hiyo inaondoa uvumi ambao
umekuwapo kwa takriban miezi mitatu sasa
kwamba naye tayari ameingia katika
kinyang’anyiro hicho.
Pinda aliweka wazi nia ya kuelekea Ikulu
akisisitiza kuwa hajatangaza rasmi lakini
akasema kuwa ameanza harakati hizo
‘kimyakimya’. Alikuwa akijibu moja ya
maswali aliyoulizwa katika Kipindi cha Dira
ya Dunia kinachorushwa na Shirika la
Utangazaji la Uingereza (BBC).
Alitamka rasmi kuwania nafasi hiyo baada ya
kuulizwa kuwa anafikiri ni kiongozi gani
anayefaa kurithi mikoba itakayoachwa na
Rais Jakaya Kikwete.
“Mikoba ya Rais Kikwete inaweza
kuchukuliwa na yeyote atakayeonekana
mwisho wa safari kwa utaratibu wa chama na
ndani ya Serikali .... kama anafaa.
Waliojitokeza sasa ni wengi na mimi
ninadhani ni vizuri,” alisema Pinda.
Alipoulizwa kama yupo miongoni mwa wengi
alisema, “… umesikia kama nimo … basi
tukubali hilo na yeye Waziri Mkuu yumo. Hao
wote waliojitokeza pamoja na Waziri Mkuu
aliyejitokeza ni katika jitihada za kusema
hebu Watanzania nitazameni je, mnaona
nafaa au hapana?”

Wednesday, October 22, 2014

MAKAMBA AHAHIDI KUMPIGIA DEBE MWANAE MBIO ZA URAISI 2015

Mbio za urais ndani ya CCM zimechukua sura mpya baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba kutangaza rasmi kumuunga mkono mtoto wake, January Makamba.

Akizungumza katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Tegeta, Dar es Salaam, Mzee Makamba alisema ameamua kumuunga mkono January kwa sababu anaamini mwanaye ana uwezo.

“Mbali ya kwamba January ni mwanangu, lakini najua ana uwezo, anajua shida za Watanzania kwa kuwa alikuwa msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete ambaye walizunguka naye Tanzania na dunia nzima.

“Makamba ni msomi, kijana na Tanzania ya sasa inahitaji rais wa kisasa atakayekwenda na kasi ya dunia na Junuary ni kizazi cha digitali, siyo kizazi cha BBC yaani Born Before Computer ambao hawana uwezo wa kukabiliana na kasi ya dunia ya leo,” alisema.

Mzee Makamba alisema ameamua kufunguka kuhusu msimamo wake huo, baada ya watu wengi kumuuliza anamuunga mkono nani kati ya wagombea waliotangaza nia na ambao bado hawajatangaza.

Alitoa mfano wa mti wa mkomamanga kuwa huzaa komamanga na kwamba yeye atamuunga mkono mtoto wake badala ya mtu mwingine.

KIBOKO YANGU YA FA IPO ON AIR

Msanii wa hip hop bongo mwanafalsafa a.k.a FA leo amedondosha kibao chake kipya kiendacho kwa jina la kiboko yangu akimshilikisha Ali Kiba. Bravoooo FA.

R.I.P YP

Msanii YP Leo ameagwa rasmi katika viwanja vya TCC Chang'ombe na kuzikwa rasmi. Ulale salama Boy

Sunday, October 19, 2014

MKALI DIAMOND AKIFANYA YAKE KWA JUKWAA

Thursday, October 9, 2014

KURA YA MAONI YA KATIBA NJIA PANDA

Rais Jakaya Kikwete jana alipokea Katiba inayopendekezwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, na papo hapo kurejesha mpira kwa viongozi wa Serikali kutafuta njia za kukamilisha mchakato huo.
Bunge la Katiba lilikamilisha kazi yake ya kuandika Katiba mpya Oktoba 2 kwa kukamilisha upigaji wa kura za kupitisha  asimu ya Katiba ambayo ilitakiwa ipitishwe kwa theluthi mbili ya kura kutoka kila upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sunday, October 5, 2014

YANGA YAWAPIGISHA KWATA JKT

Kikosi cha timu ya Young Africans chini ya kocha mbrazil Marcio Maximo leo kimeendeleza wimbi
la ushindi katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya maafande wa jeshi la
Kujenga Taifa nchini JKT Ruvu mchezo uliofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijin
Dar es salaam.