Hii ilikuwa ni katika droo ya ufunguzi wa kombe la FIFA Confederation la mwaka 2013 iliofanyika huko Sao Paul Brazili katika ukumbi wa Anhambi. Katika droo hiyo timu ya taifa ya Brazil inategemea kukipiga na timu ya taifa ya Italy, wakati Spain atakipiga na Uruguay.
Kundi A litakuwa kama ifuatavyo: Brazil, Japan, Mexico na Italy.
Kundi B litajumuisha timu ya Spain, Uruguay, Tahiti na watakaokuwa mabingwa wa Afrika. Mashindano haya yatapigwa huko Brazil kuanzia tarehe 15-30 ya mwezi juni mwaka 2013. Na haya ni mashindano ya tisa tangu kuanzishwa kwake na FIFA.
Kufanyika kwa mashindano haya ni maandalizi ya kombe la dunia litakalo fanyika hukohuko Brazili ifikapo mwaka 2014.