Sunday, May 12, 2013

JE WAJUA, HEWA YA UKAA YAONGEZEKA DUNIANI?

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya mwanadamu kipimo cha kiwango cha hewa ya Ukaa kuongezeka na kufikia mia nne kwa milioni moja ya sehemu za dunia. Kwa mujibu wa takwimu za maabala ya serikali ya Marekani huko Hawaii, wamesema kiwango hicho kimekuwa kutokana na sababu mbalimbali. Mara ya mwisho hewa na Ukaa kufikia kiwango cha juu ilikuwa miaka milioni tatu hadi milioni tano iliyopita ambapo ilikuwa chiniya mia nne kwa sehemu milioni moja za dunia(400ppm) Wanasayansi hao wanasema pia kiwango cha joto kimezidi maradufu kuliko miaka iliyopita. Hewa ya Ukaa inatajwa kama gesi inayotengenezwa zaidi na binadamu ambapo imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa uongezekaji wa joto duniani kwa miaka mingi. Wanaharakati wa masuala ya mazingira wamesema hatua hii ni pigo kubwa na kuonyesha wazi madhara ya mabadiliko ya tabia nchi. Lakini wanaharakati hao wanasema vifaa vya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi vimeandiliwa na kupambana na tatizo hilo.
By BBC SWAHILI

Sent from my Windows® phone.

0 comments: