Maafisa wa hospitali mjini Benghazi nchini Libya wanasema kiasi ya watu ishirini na saba wameuawa huku wengine hamsini wakiwa wamejeruhiwa katika mapigano kati ya waandamanji na wapiganaji wanaoungwa mkono na wizara ya ulinzi nchini humo. Wakazi wa mji huo wanasema ghasia zilizuka baada ya mamia ya waandamanji kukusanyika nje ya makao makuu ya jeshi la ulinzi nchini humo wakitaka wapiganaji hao kuondoshwa, Jambo ambalo wizara hiyo inakataa kufanya. Milio ya risasi ilisikika huku watu wakimbia kutafuta kujihifadhi. Bado Libya inatarajia kujenga upya jeshi la kisawa sawa tangu kuondoshwa madarakani kanali Muammar Gaddafi na kuwepo wapiganaji ambao wanaziba pengo hilo lakini umma unazidi kuwapinga.
Frm bbcswahili
0 comments:
Post a Comment