Sunday, December 15, 2013

BURIHANI MADIBA

Mandela amezikwa kuambatana na tamaduni za Xhosa.Ng’ombe dume amechinjwa, na jeneza la hayati
Mandela kufungwa kwa ngozi ya Chui huku mzee
mmoja wa familia akiongea na mizimu ya mfu
hadi Madiba alipozikwa.Mazishi ya Mandela pia yamejumuisha tamaduni za watu wa jamii ya Xhosa ambako ukoo wa
Mandela wa Thembu unatoka.
Bila shaka mazishi ya Mandela katika kijiji cha Qunu yamekuwa mchanganyiko wa mila na
tamaduni , dini ya kikristo na pia watakaofika katika  mazishi ya kitaifa.
Watu wa jamii ya Xhosa ambao ni moja ya kabila
kubwa zaidi Afrika Kusini ikiwa na watu milioni saba wanatoka Kusini Mashariki mwa nchi katika mkoa wa Cape Mashariki.
Watu wa kabila la Xhosa wanatambua mizimu ya
mababu zao na wao huzungumza nayo wakati
wakitaka msaada.
Wanaamini kuwa lazima mwili ujulishwe
kinachofanyika kabla ya kuuzika
Wanasema kuwa Madiba Lazima afahamishwe
Jumapili kuwa anazikwa .
Lazima jeneza lake litafungwa kwa ngozi ya Chui
kwa sababu alikuwa mtoto wa mfalme wa kitamaduni.
Lakini kwa sababu Madiba alikuwa Rais wa
zamani , lazima pawepo bendera ya nchi. Bila
shaka hii ni ishara ya heshima kwa kiongozi
mheshimiwa.
Ng’ombe atachinjwa mapema alfajiri na kuliwa na
watu waliofika kwa maombolezi. Na baada ya
mwaka mmoja tangu kuzikwa kwa Madiba,
Ng’ombe mwingine atachinjwa na kuliwa na
familia ishara kuwa maombolezi yamekwisha.

0 comments: