KARIBU BONGO CORNER ENTERTAINMENT GROUP

Karibu katika site yako iliyo bora na inayokuletea habari mbalimbali zinazoigusa dunia katika nyanja ya burudani zaidi. Kaa mkao wa kuburudika zaidi ndani ya Bongo Corner!!! More

Friday, October 24, 2014

FISI AZUA KIZAAZAA MJINI SINGIDA

Leo katika mji wa Singida eneo lifaamikalo kama sokoni aliibuka fisi na kuzua mtafaruku. Fisi huyo ambaye baada ya watu kumzonga aliingia katika moja ya duka lililokuwa wazi. Wananchi waliokuwapo eneo hilo walifanikiwa kumpiga fisi huyo na hatimaye kumuua kabisa. Ila chaajabu watu wengi wamekuwa wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina kwani ni ajabu fisi kutokea katikati ya mji ambapo hamna ata mbuga karibu. ...

Thursday, October 23, 2014

WAZILI MKUU MIZENGO PINDA NAYE AFUNGUKA KUHUSU KUGOMBEA URAISI

Siyo tetesi tena. Sasa ni rasmi kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amekuwa akitajwa kuwania urais amethibitisha wazi kuwa atagombea kiti hicho katika uchaguzi mkuu mwakani. Alitoa uthibitisho huo juzi akiwa London, Uingereza ambako yuko katika shughuli za kikazi. Hatua hiyo inaondoa uvumi ambao umekuwapo kwa takriban miezi mitatu sasa kwamba naye tayari ameingia katika kinyang’anyiro hicho. Pinda aliweka wazi nia ya kuelekea Ikulu akisisitiza...

Wednesday, October 22, 2014

MAKAMBA AHAHIDI KUMPIGIA DEBE MWANAE MBIO ZA URAISI 2015

Mbio za urais ndani ya CCM zimechukua sura mpya baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba kutangaza rasmi kumuunga mkono mtoto wake, January Makamba. Akizungumza katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Tegeta, Dar es Salaam, Mzee Makamba alisema ameamua kumuunga mkono January kwa sababu anaamini mwanaye ana uwezo. “Mbali ya kwamba January ni mwanangu, lakini najua ana uwezo, anajua shida za Watanzania kwa kuwa alikuwa msaidizi...

KIBOKO YANGU YA FA IPO ON AIR

Msanii wa hip hop bongo mwanafalsafa a.k.a FA leo amedondosha kibao chake kipya kiendacho kwa jina la kiboko yangu akimshilikisha Ali Kiba. Bravoooo FA. ...

R.I.P YP

Msanii YP Leo ameagwa rasmi katika viwanja vya TCC Chang'ombe na kuzikwa rasmi. Ulale salama Boy ...

Sunday, October 19, 2014

MKALI DIAMOND AKIFANYA YAKE KWA JUKWAA

...

Thursday, October 9, 2014

KURA YA MAONI YA KATIBA NJIA PANDA

Rais Jakaya Kikwete jana alipokea Katiba inayopendekezwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, na papo hapo kurejesha mpira kwa viongozi wa Serikali kutafuta njia za kukamilisha mchakato huo. Bunge la Katiba lilikamilisha kazi yake ya kuandika Katiba mpya Oktoba 2 kwa kukamilisha upigaji wa kura za kupitisha  asimu ya Katiba ambayo ilitakiwa ipitishwe kwa theluthi mbili ya kura kutoka kila upande wa Jamhuri ya Muungano...

Sunday, October 5, 2014

YANGA YAWAPIGISHA KWATA JKT

Kikosi cha timu ya Young Africans chini ya kocha mbrazil Marcio Maximo leo kimeendeleza wimbi la ushindi katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya maafande wa jeshi la Kujenga Taifa nchini JKT Ruvu mchezo uliofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijin Dar es salaam. ...