KARIBU BONGO CORNER ENTERTAINMENT GROUP

Karibu katika site yako iliyo bora na inayokuletea habari mbalimbali zinazoigusa dunia katika nyanja ya burudani zaidi. Kaa mkao wa kuburudika zaidi ndani ya Bongo Corner!!! More

Saturday, December 9, 2017

RAISI ATOA MSAMAHA KWA PAPII KOCHA NA BABU SEYA

Raisi Dkt. John Magufuli ametoa msamaha kwa wasanii Papii Kocha na Nguza Viking a.k.a Babu Seya waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela.
Raisi Magufuli ameyasema hayo mapema leo alipokuwa anahutubia katika sherehe za kuazimisha miaka 56 ya uhuru wa Tanganyika.

Friday, November 10, 2017

Maisha popote

Oi oi

Thursday, September 21, 2017

DIAMOND APATA MCHONGO MWINGNE

Msanii wa bongo flava Diamond platinumz amepata mchongo mwingine wa kuwa balozi wa brand kubwa ya wine toka Ufaransa, Belaire. Hii inamfanya Diamond kuwa mmoja kati ya mabarozi 200 wa wine hiyo. Big up Simba!!!

Wednesday, June 28, 2017

KIJANA RAYVAN ATEGEMEWA KUTUA LEO TWENZETU

Hongera sana Rayvan na karibu sana home tena kwa kishindo kikubwa. Umeiwakilisha vyema Tz bro!

Monday, May 29, 2017

IGP SIMON SIRRO ALIVYOAPISHWA IKULU

Raisi wa Tanzania Dkt.  John Magufuli akimuapisha aliyekuwa kamishna wa polisi kamanda Simon Sirro kuwa mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP) Tanzania.

Monday, May 8, 2017

BANKI KUU YA TANZANIA YAIFUTIA LESENI BENKI YA FBME

Banki Kuu ya Tanzania imesimamisha shughuli zote za FBME Bank Limited ikiwemo kufuta leseni yake ya kufanya shughuli za kibenki; kuiweka chini ya ufilisi; na kuiteua Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kama mfilisi kuanzia tarehe 8 Mwezi Mei, 2017 


Miili ya wanafunzi walimu na dereva yawasili uwanjani

Miili ya wanafunzi, walimu na dereva waliopata ajali imewasili uwanjani, ililetwa na magari ya Jwtz kwaajili ya kuagwa rasmi.

Wabunge watoa posho zao kuomboleza vifo vya wanafunzi

Wabunge wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania watoa posho zao kwaajili ya kuomboleza vifo vya wanafunzi.

Saturday, March 25, 2017

SAMATTA AING'ARISHA TAIFA STARS



Timu ya Taifa "Taifa Stars" imeifunga timu ya Botswana mabao 2 kwa 0 katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyuochezwa leo katika uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Mabao ya Taifa Stars yametiwa nyavuni na Mbwana Samatta, bao la kwanza likifungwa mapema kabisa dakika ya pili ya mchezo na bao la pili likiingia nyavuni dakika 87 ya mchezo.

Monday, March 20, 2017

RAISI AMTAKA RC MAKONDA APIGE KAZI

Raisi Magifuli amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kuendelea kupiga kazi kama sehemu ya majukumu yake.

"Mimi ni rais ninayejiamini, sipangiwi mambo ya kufanya. Hata fomu ya kugombea nilikwenda kuichukua peke yangu, kwa hiyo Makonda wewe chapa kazi," amesema Rais Magufuli.

Thursday, March 16, 2017

CAF YAPATA RAISI MPYA

Mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa miguu Madagasca bwana Ahmad ameshinda uchaguzi wa kinyang'anyilo cha uraisi wa CAF na kumbwaga aliyekuwa raisi wa chama hicho Hayatou toka Cameroon aliyeshikilia nafasi hiyo tangu mwaka 1988.




RAISI MAGUFULI ATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA IKULU DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wametembelea eneo linalofanyakazi za ufyatuaji wa Matofali yatakayotumika katika ujenzi wa Ikulu Chamwino huko mkoani Dodoma.

Wednesday, March 15, 2017

TRA YATIA KUFURI OFISI ZA TFF

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) limezifungia Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na madai ya kodi inayodaiwa shirikisho hilo.
Tukio hilo la kufungiwa ofisi na TRA limefanywa kupitia Kampuni ya udalali ya yono Auction Mart imewataka wafanyazi kuacha kila kitu cha shirikisho hilo ndani ya ofisi.
Tupe maoni yako

Monday, March 13, 2017

KANTE AIUA MAN UNITED

N'golo Kante' mchezaji mwenye jezi nambari 7 mgongoni ameiwezesha timu ya chelsea kuvuka robo fainali baada ya kuifunga timu ya Man United bao moja kwa nunge dakika ya 51 ya mchezo.

MAN U AU CHELSEA LEO?

Nani kutoka kidedea leo ikiwa zimebaki dakika chache mpira kuwekwa katikati kati ya Man United na Chelsea?

Sunday, March 12, 2017

Sir George Kahama afariki dunia

Aliyekuwa waziri wa kwanza wa mambo ya ndani katika serikali ya awamu ya kwanza ya Hayati Mwl Nyerere, Sir George Kahama amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa ya muhimbili alipokuwa anapata matibabu.

Wednesday, March 8, 2017

BARCA NOMA WAICHAPA PSG 6-1

Timu ya Barcelona imeichakaza timu ya Paris Saint Germain (PSG) mabao 6-1 katika mashindano yanayoendelea ya UEFA.
Mchezaji Sergi Roberto alifunga bao la 6 kwa mkwaju wa mwisho wa mchezo, na hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 6-5 kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Nou Camp.
Barcelona walifunga magoli matatu katika dakika saba za mwisho. Walikuwa wakiongoza kwa 3-1.


Wiki tatu zilizopita PSG iliifunga Barcelona magoli 4-0 mjini Paris.
Hatua ya kurejesha magoli yote hayo ni kubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya UEFA, na sasa Barcelona wana kila nafasi ya kunyanyua kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.

Wednesday, March 1, 2017

RAISI AMTEUA MAMA SALMA KIKWETE KUWA MBUNGE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Magufuli amemteua Mhe. Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.