Timu ya Barcelona imeichakaza timu ya Paris Saint Germain (PSG) mabao 6-1 katika mashindano yanayoendelea ya UEFA.
Mchezaji Sergi Roberto alifunga bao la 6 kwa mkwaju wa mwisho wa mchezo, na
hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 6-5 kwenye mchezo uliopigwa kwenye
dimba la Nou Camp.
Barcelona walifunga magoli matatu katika dakika saba za mwisho. Walikuwa wakiongoza kwa 3-1.
Wiki tatu zilizopita PSG iliifunga Barcelona magoli 4-0 mjini Paris.
Hatua
ya kurejesha magoli yote hayo ni kubwa kuwahi kushuhudiwa katika
historia ya UEFA, na sasa Barcelona wana kila nafasi ya kunyanyua kombe
la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.
0 comments:
Post a Comment