KARIBU BONGO CORNER ENTERTAINMENT GROUP

Karibu katika site yako iliyo bora na inayokuletea habari mbalimbali zinazoigusa dunia katika nyanja ya burudani zaidi. Kaa mkao wa kuburudika zaidi ndani ya Bongo Corner!!! More

Saturday, March 25, 2017

SAMATTA AING'ARISHA TAIFA STARSTimu ya Taifa "Taifa Stars" imeifunga timu ya Botswana mabao 2 kwa 0 katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyuochezwa leo katika uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Mabao ya Taifa Stars yametiwa nyavuni na Mbwana Samatta, bao la kwanza likifungwa mapema kabisa dakika ya pili ya mchezo na bao la pili likiingia nyavuni dakika 87 ya mchezo.

Monday, March 20, 2017

RAISI AMTAKA RC MAKONDA APIGE KAZI

Raisi Magifuli amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kuendelea kupiga kazi kama sehemu ya majukumu yake.

"Mimi ni rais ninayejiamini, sipangiwi mambo ya kufanya. Hata fomu ya kugombea nilikwenda kuichukua peke yangu, kwa hiyo Makonda wewe chapa kazi," amesema Rais Magufuli.

Thursday, March 16, 2017

CAF YAPATA RAISI MPYA

Mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa miguu Madagasca bwana Ahmad ameshinda uchaguzi wa kinyang'anyilo cha uraisi wa CAF na kumbwaga aliyekuwa raisi wa chama hicho Hayatou toka Cameroon aliyeshikilia nafasi hiyo tangu mwaka 1988.
RAISI MAGUFULI ATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA IKULU DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wametembelea eneo linalofanyakazi za ufyatuaji wa Matofali yatakayotumika katika ujenzi wa Ikulu Chamwino huko mkoani Dodoma.

Wednesday, March 15, 2017

TRA YATIA KUFURI OFISI ZA TFF

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) limezifungia Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na madai ya kodi inayodaiwa shirikisho hilo.
Tukio hilo la kufungiwa ofisi na TRA limefanywa kupitia Kampuni ya udalali ya yono Auction Mart imewataka wafanyazi kuacha kila kitu cha shirikisho hilo ndani ya ofisi.
Tupe maoni yako

Monday, March 13, 2017

KANTE AIUA MAN UNITED

N'golo Kante' mchezaji mwenye jezi nambari 7 mgongoni ameiwezesha timu ya chelsea kuvuka robo fainali baada ya kuifunga timu ya Man United bao moja kwa nunge dakika ya 51 ya mchezo.

MAN U AU CHELSEA LEO?

Nani kutoka kidedea leo ikiwa zimebaki dakika chache mpira kuwekwa katikati kati ya Man United na Chelsea?