KARIBU BONGO CORNER ENTERTAINMENT GROUP

Karibu katika site yako iliyo bora na inayokuletea habari mbalimbali zinazoigusa dunia katika nyanja ya burudani zaidi. Kaa mkao wa kuburudika zaidi ndani ya Bongo Corner!!! More

Sunday, December 15, 2013

BURIHANI MADIBA

Mandela amezikwa kuambatana na tamaduni za Xhosa.Ng’ombe dume amechinjwa, na jeneza la hayati
Mandela kufungwa kwa ngozi ya Chui huku mzee
mmoja wa familia akiongea na mizimu ya mfu
hadi Madiba alipozikwa.Mazishi ya Mandela pia yamejumuisha tamaduni za watu wa jamii ya Xhosa ambako ukoo wa
Mandela wa Thembu unatoka.
Bila shaka mazishi ya Mandela katika kijiji cha Qunu yamekuwa mchanganyiko wa mila na
tamaduni , dini ya kikristo na pia watakaofika katika  mazishi ya kitaifa.
Watu wa jamii ya Xhosa ambao ni moja ya kabila
kubwa zaidi Afrika Kusini ikiwa na watu milioni saba wanatoka Kusini Mashariki mwa nchi katika mkoa wa Cape Mashariki.
Watu wa kabila la Xhosa wanatambua mizimu ya
mababu zao na wao huzungumza nayo wakati
wakitaka msaada.
Wanaamini kuwa lazima mwili ujulishwe
kinachofanyika kabla ya kuuzika
Wanasema kuwa Madiba Lazima afahamishwe
Jumapili kuwa anazikwa .
Lazima jeneza lake litafungwa kwa ngozi ya Chui
kwa sababu alikuwa mtoto wa mfalme wa kitamaduni.
Lakini kwa sababu Madiba alikuwa Rais wa
zamani , lazima pawepo bendera ya nchi. Bila
shaka hii ni ishara ya heshima kwa kiongozi
mheshimiwa.
Ng’ombe atachinjwa mapema alfajiri na kuliwa na
watu waliofika kwa maombolezi. Na baada ya
mwaka mmoja tangu kuzikwa kwa Madiba,
Ng’ombe mwingine atachinjwa na kuliwa na
familia ishara kuwa maombolezi yamekwisha.

Saturday, December 7, 2013

MANDELA KUZIKWA DISEMBA 15

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa Hayati Nelson Mandela atazikwa tarehe kumi na tano Jumapili mwezi Disemba katika kijiji cha Qunu mkoa wa Eastern Cape.

name BBC Swahili

Friday, December 6, 2013

NELSON MANDELA AAGA DUNIA

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ameaga dunia.
Mandela amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.
Taarifa zinazohusiana
Afrika Kusini
Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.
Mnamo mwaka 2005, Mandela alitangaza kwa taifa kuwa mwanawe wa kume alifariki kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kuondoka gerezani.
Hakuonekana sana hadharani tangu alipostaafu mwaka 2004.