Wednesday, February 22, 2012

Mwanamke wa Wiki

Flaviana Matata mwanamitindo wa kike anayetikisa nje ya bongo na kuifanya Tanzania kung'ara katika tasnia ya mitindo kimataifa. Leo mrembo huyu mwanamitindo ndiye anayetung'arishia ukurasa wetu kwa kuwa ni mwanamke wa wiki ndani ya Bongo Corner. Hii ndiyo aina ya wanawake wanaoitajika katika dunia ya leo yaani kwa maana kwamba, mwanamke anapaswa kujishughulisha na siyo kungojea kuwa mdakaji. Flaviana ni moja kati ya hawa wanawake ninao wazungumzia. Mwanadada huyu kwa sasa anamiliki au anatarajia kumiliki taasisi yake inayofahamika kama Flaviana Matata Foundation. Pongezi za dhati kabisa zinadondoka kwako mwanadada Flaviana toka katika uongozi mzima wa Bongo Corner Entertainment na Mungu akuzidishie katika kazi zako!

0 comments: