Wednesday, February 22, 2012

Sugu na Ruge sasa Amani

Meza kuu ya upatanisho ilikaliwa na Mhe. Emanuel Nchimbi wazili  wa vijana, habari,michezo na utamaduni, Joseph Mbilinyi (sugu) mbunge wa Mbeya mjini, Ruge Mutahaba (Mkurugenzi wa Clouds Media Group) na mbunge wa Singida mashariki Mhe. Tundu Lisu.
Hii ilikuwa katika kutafuta suluhisho la mafarakano yaliokuwepo kati ya Mr. Sugu na Mr. Ruge yaliyofanyika mbele ya waandishi wa habari kwa lengo moja tu la kutafuta huo upatanishi. Sasa Sugu na Ruge wanafungua ukurasa mpya na kufuta yale yaliyopita. Waswahili husema "Yaliyopita si ndwele tugange yajayo"  na sasa tunategemea kuona kauli mpya tofauti na zile zilizopita. Amani kwenu wadau.

0 comments: