Saturday, February 11, 2012

Rooney aipaisha Man United!

Mabao mawali yaliyofungwa na Wyne Rooney yameipa Manchester United ushindi zidi ya maasimu wao Liverpool katika uwanja wa Old Trafford. Ushindi huo umeifanya timu ya Manchester United kukaa kileleni kwa sasa huku mechi ya maasimu wao wakuu Manchester City ikiwa inasubiriwa kuthibitisha uwepo wao kileleni.
hekaheka kati ya Evra(Manchester United) na Suarez (Liverpool) halikukosekana, ni kutokana na Suarez kukataa kumpa mkono wa kheri Evra kabla ya mech kuanza na Evra kuutupilia mbali mkono wa Suarez alipokuwa akimsalimia goli kipa wa Manchester United (De Gea).
Mpira ulianza kwa kasi kubwa sana huku Manchester United wakioneka na kuumilika mpira kwa hali ya juu lakini mpaka timu zinakwenda mapumziko mabao yalikuwa ni bila kwa bila. Upepo ulikuja kubadilika katika kipindi cha pili dakika ya 47 ambapo Rooney aliipa timu yake bao la kwanza. Mnamo dakika ya 50 Wyne Rooney hakufanya hajizi kwa kuipa tena timu yake bao la pili, lakini ilipofika dakika ya pili Luic Suarez aliipatia Liverpool bao la kwanza ukiwa ni mpira uliochezwa vibaya na beki tegemezi ya Manchester United Ferdinand na Suarez kuusukumia mpira huo wavuni.
Ushindi huo unaipa Manchester Unnited pointi 58 zidi ya 57 ya Manchester City, ikifuatiwa na Tottenham yenye pointi 53 zidi ya Arsenal yenye pointi 43 ikilingana na Chelsea kwa poinnti na wengine wakifuatia.

0 comments: