Saturday, February 11, 2012

Whitney Afariki dunia!

Whitney Huston enzi za uhai wake
Kwa habari zilizotufikia ni kwamba msanii Whitney Huston amefariki dunia, habari toka CNN zilisema kuwa mkali huyo alikutwa na umauti  mida ya 3:55 p.m katika hotel ijulikanayo kama Beverly Hilton Hotel.
Huston amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48 tangu kuzaliwa kwake mwaka 1964.
Whitney atakumbukwa kwa kazi nyingi alizozifanya enzi za uhai wake, hususani albamu zake mbili za ukweli  kama "I'm your Baby Tonight," ya miaka ya 90 na "The Bodyguard" kazi iliyotufanyika miaka ya 92.
Salamu za pole ziende kwa wapenzi wote wa mwana mziki huyo hususani kwa yake familia na hasa mwanae wa kike afahamikaye kama Bobbi Kristina. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina!









0 comments: