Monday, September 29, 2014

TBS YAZUIA UVAAJI WA NGUO ZA MITUMBA

Shirika la Viwango (TBS) limewataka
wananchi kutonunua nguo za ndani za mtumba ili
kuua soko la bidhaa hizo zenye athari kiafya.
Kaimu mkurugenzi anayehusika na udhibiti ubora
wa TBS, Mary Meela alisema nguo hizo ni hatari
kwani zinaweza kueneza magonjwa mbalimbali
hasa ya ngozi.
Alisema lengo la ombi hilo ni kukomesha uuzaji
wa nguo hizo ambazo zinaweza kusababisha
maambukizi kutoka kwa aliyekuwa anavaa nguo
hiyo kwenda kwa mtu wa pili.
Meela alisema shirika lake linashindwa
kukomesha biashara hiyo kwa sababu halijapewa
nguvu za kisheria kukataza watu kufanya
biashara hiyo kama ilivyo Zanzibar, hivyo
amewataka wananchi kutambua madhara hayo na
kuacha kununua.
“Nguo za ndani zina bei ndogo hata mtu wa chini
anaweza kumudu. Sioni sababu ya mtu kwenda
kununua za mtumba,” alisema.

Info frm mwananchi communication ltd

0 comments: