Monday, February 16, 2015

Sitta amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu TPA

Waziri wa Uchukuzi
Samuel Sitta amemsimamisha kazi
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni
Kipande baada ya kuwepo malalamiko
ya ubabaishaji katika zabuni mbalimbali
za mamlaka hiyo.
Hatua hiyo ya Sitta imekuja wiki tatu
baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya
Kikwete kuiongoza wizara hiyo akitokea
Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla,
wizara hiyo ilikuwa chini ya Dk
Harrison Mwakyembe.

0 comments: