Sunday, March 1, 2015

BURIANI CAPT KOMBA

Mbunge wa Mbinga Magharibi
na Mkurugenzi wa Kikundi cha
Tanzania One Theatre (TOT) Kapteni
John Komba amefariki dunia jana
alipokuwa akipelekwa katika hospitali
ya TMJ jijini Dar es Salaam baada ya
kuzidiwa.
Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na
Hospitali ya TMJ, ofisi ya Bunge na
Chama Cha Mapinduzi na kwamba kwa
sasa taratibu za maziko yake
zinaendelea kufanywa .
Aidha taarifa za kutoka
nyumbani kwake maeneo ya Mbezi
Beach Tangi Bovu zinaeleza kuwa
maelfu ya watu kutoka katika kada
mbalimbali wanaendelea kumiminika
nyumbani kwa marehemu ili kutoa
faraja kwa familia kwani marehemu
ameacha mjane mmoja na watoto kumi
na moja.
Akizungumza na tovuti hii mmoja wa
madaktari aliyempokea wakati
anafikishwa hospitali ya TMJ, Dk Elisha
Ishan amesema Komba alifikishwa
hospitalini hapo saa 10 jioni leo akiwa
mahututi .
"Nilimpokea nilianza moja kwa moja
kumpima shinikizo la damu na vipimo
vingine lakini tayari vilikuwa havifanyi
kazi na hapo ndipo tukathibitisha kuwa
ndugu yetu ameaga dunia," amesema Dk
Ishan
Pamoja na hayo Dk Ishan amekwepa
kutaja moja kwa moja chanzo cha kifo
cha mareheme, hata hivyo amesema
Kapteni Komba alikuwa na tatizo la
shinikizo la damu na kwamba siku za
karibuni alifika hospitalini hapo kwenye
kiliniki yake ya shinikizo la damu

0 comments: