Monday, November 26, 2012

SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA

Kwa habari toka kwa kamanda wa polisi mkoani Tanga zinasema kuwa Sharo milionea amefariki baada ya gari alilokuwa anaendesha kuacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake. Akizungumza na vyombo vya habari kamanda alikuwa na haya yakusema,"leo majira ya sa a mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza" Inasemekana kuwa katika eneo alilopata ajali hakukuwa na kona kali sana wala ubovu wa barabara, katikati ya Segera na Muheza na gari lake imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.Katika gari hilo Sharo alikuwa pekeyake. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU AMAHALI PEMA PEPONI AMINA!

0 comments: