Saturday, October 13, 2012

DIAMOND AIPIGIA PROMO NGORONGORO CRATER

 Msanii Naseeb Abdul akiwa pande za mbuga ya Ngorongoro katika kulinadi bonde la Ngorongoro ili liweze kushinda katika mashindano ya maajabu saba ya dunia.
Akizungumza na vyombo vya habari Diamond The Platinumz alikuwa na haya ya kusema:“Hii ni mara yangu ya kwanza kufika hapa, lakini kwa kweli nimeshangazwa na jinsi palivyo pazuri, wanyama, mito ambayo inapita huku chini, mi huwa naona kwenye televisheni tu katika kile kipindi cha National Geography cha DSTV lakini sikujua kama mambo haya yapo kweli kwetu. “Nawaomba watanzania wenzangu waweze kutembelea Ngorongoro na vivutio vyetu vya utalii kwa sababu kuna mengi ya kujifunza, leo kama isingekuwa Afrika sidhani kama kungekuwa na kipindi kama National Geography, na gharama za kuja huku si kubwa, hatupaswi kuogopa, hivi ni vitu ambavyo vinawezekana kabisa suala ni kujipanga,”


0 comments: