Saturday, August 18, 2012

ARSENAL,SUNDERLAND WACHOSHANA NGUVU KATIKA EPL 2012/13

Mshikemshike ndani ya uwanja wa Emirates jijini London kati ya Arsenal na Sunderland umeisha kwa timu zote mbili kuishia kuchoshana nguvu kwa kutoka na sale ya bila kwa bila. Mchezo huu mmoja wapo wa ufunguzi wa michuano ya ligi kuu Uingereza, umeshuhudiwa na mashabiki wapatao 60078 na kuchezeshwa na refalii C, Foy.
Na huko katika viwanja vingine Fulham kampiga Norwich City mabao matano(5) kwa sifuri(0) mchezo uliochezwa katika uwanja wa Craven Cottage, Swansea City imempiga QPR mabao matano kwa sifuri, mchezo uliochezwa uwanja wa Loftus Road. Stock City nae katoka na Reading mojamoja. Liverpool kachapika mabao matatu(3) kwa sifuri (0) toka kwa West Bromwhich na West Ham imempiga Aston Villa bao moja katika uwanja wa Boleyn.

0 comments: