Thursday, August 16, 2012

VAN PERSIE ATUA KATIKA KLABU YAKE MPYA YA MANCHESTER UNITED

Umekuwa ni kama mzimu unaoendelea kuitafuna timu ya Arsenal ndani ya miaka saba sasa tangu mwaka 2005. Klabu ya Arsenal mpaka sasa imeshawauza majembe yake ya kutegemewa kama, Patrick Vieira, Thierry Henry, Cesc Fabregas na sasa Van Persie.
Van Persie ni mchezaji pekee toka Arsenal kuweka uelekeo wake kuwa klabu ya Manchester. Haitasahaulika kuwa Wenger na Ferguson ni mahasimu wakubwa katika jiji la London, lakini hii leo wanafanya bihashara pasipo shida. Van Persie amenunuliwa kwa kiasi cha euro milioni 30, kuichezea Man United kwa mkataba wa miaka minne kama alivyosema bosi wa Arsenal, Arsene Wenger. Kazi kwenu Man United!

BC Crew

0 comments: