Sunday, December 23, 2012

FERGUSON ALIA NA MUAMUZI

Meneja wa timu ya Manchester, Sir Alex Ferguson amelalamikia uamuzi mbovu wa mpuliza kipenga aliyechezesha mechi kati ya Man United na Swansea City iliyochezwa jana jumapili. Meneja wa Man United Sir Alex Ferguson amelalamika kuwa huenda mchezaji wake Robin Van Persie angefikwa na umauti baada mchezaji wa Swansea, Ashley Williams kumpiga RVP mpira wa kichwa na muamuzi kutochukua atua zozote.
Akizungumza na Sky Sports, boss wa United alisisitiza kuwa ile ilikuwa ni foul ya wazi kabisa lakini muamuzi Michael Oliver aliimezea.
Ferguson aliendelea kusema,"natambua muamuzi ni kijana bado lakini nimekatishwa tamaa na utendaji kazi wake. Tukio la Van Persie aliliona dhahiri."

BC Crew

0 comments: