Friday, May 24, 2013

KLABU BINGWA ULAYA KUMEKUCHA

Zilikuwa siku na sasa ni masaa machache tu yamebaki ili kutanabai nani ni kinala wa soka Ulaya.
Dortmund au Bayern Munich?, hilo ndilo swali vichwani mwa mashabiki wa soka Duniani kwa sasa.
Jaramba linapigiwa katika uwanja wa Wembley nchini Uingereza, huku vilabu vyote vya uingereza vikiwa nje ya mashindano hayo na kubakia kuwa watazamaji tu siku ya leo.
Fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza, inahusisha timu mbili kutoka Ujerumani, wachambuzi wa soka wanadai hii ni ishara ya ufanisi wa ligi kuu ya Bundesliga ya kuwekeza katika kukuza vipaji hasa raia wa nchi hiyo.
Takriban wachezaji wote wa timu ya taifa ya Ujerumani, watakuwa uwanjani wakati wachezaji wa Klabu ya Bayern Munich watakapotoana jasho na Borussia Dortmund, katika uwanja wa Wembley, wengi wa wachezaji hao wakiwa wametoka katika vyuo viwili vinavyomilikiwa na vilabu hivyo

0 comments: