Saturday, May 19, 2012

CHELSEA BINGWA UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2011-2012

Katika uwanja wa Allianz Arena watoto wa Di Matteo The Blues wafanya kweli baada ya kuipiga Bayern Munich mabao 4-3.
Bayern Munich ndio waliokuwa wakwanza kuifunga Chelsea mnamo dakika ya 83 kupitia mchezaji wake Thomas Muller lakini dakika mbili kabla ya dakika 90 kumalizika, Chelsea kupitia mchezaji wake mashuhuri Didier Drogba ilisawazisha na mabao kuwa 1-1.
Hii ilipelekea mechi kwenda dakika 30 za nyongeza ambazo hadi kumalizika kwa dakika hizo, timu zote ziliishia kuchoshana nguvu. Hali hii ilipelekea matuta kupigwa na hatimaye Chelsea akaibuka bingwa.
Drogba kafanikisha kupeleka ubingwa wa ufalme wa ulaya England tangu walipoukosha mwaka 2008 kule Moscow na uteja sasa basiii!.
THANK YOU DIDIER DROGBA, THANK YOU CHELSEA!!

BC Crew

0 comments: