Saturday, May 19, 2012

LIONEL MESSI NDIYE MFUNGAJI BORA WA LIGI YA MABINGWA ULAYA 2011-2012.

Mshambuliaji machachali wa timu ya Barcelona amenyakua tuzo ya kuwa ndiye mfungaji bora wa UEFA Champions League 2011-2012, kwa kufikisha magoli 14 katika mechi 11 alizofanikiwa kucheza. Messi kutokana na ushindi huu, ameifikia rekodi iliyowahi kuwekwa na mchezaji Jose Altafini mfungaji bora wa michuano ya ulaya wa mwaka 1962-1963 akitokea timu ya AC Milan.
Messi katika mechi za makundi alifanikiwa kupata mabao 2 toka kwa BATE, 3 toka kwa timu ya Plzen na bao 1 toka kwa Milan.
Katika mzunguko wa pili Messi alifanikiwa kupata mabao mengine 6 baada ya kuinyonga Bayer Leverkusen mabao hayo 6. Messi alipigilia msumari wa jahazi kwa kuongeza magoli mengine 2 na kutimiza idadi ya magoli 14 baada ya kuifunga Milan mabao hayo 2 katika robo fainali ya UEFA.
THANK YOU MESSI!!
BC Crew

0 comments: