Sunday, June 16, 2013

HABARI ZAIDI KUHUSU MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA

Taarifa za hali ya majeruhi wa mlipuko wa bomu la Soweto, Arusha Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Arusha, Dk Josiah Mlay amewamtaja marehemu wa mlipuko uliotokea jana mkutanoni Soweto, Arusha kuwa ni Judith Mushi, (46) mkazi wa Sokoni One, jijini Arusha. Mama Judith Moshi ambaye aliwahi kuwa M/Kiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Wilaya ya Arusha Mjini na mpaka mauti yanamkuta alikuwa ni Katibu wa Chama Kata ya Sokoni. Na mwi ngine ni kijana wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 15-16 asiyetambulika jina bado, ambaye alifia katika hospitali ya AICC. Dk Mlay, amesema katika tukio hilo hospitail hiyo imepokea majeruhi 10, kati yao 9 ni wanaume na mwanamke mmoja aitwaye Sharifa Jumanne, ambaye hali yake imeelezwa kuwa mbaya. Amesema kuwa katika uchunguzi wa awali imegundulika kuna kuipande cha chuma kwenye mapafu ambacho kinatokana na mlipupuko huo. Aidha, amesema kuwa majeruhi mwingine aliyepata majeraha ya kichwa amehamishiwa kwenye hospitali ya Seliani ya Arusha kwa uchunguzi zaidi akisubiriwa kupelekwa kwenye hospitali ya rufani ya KCMC, Moshi. Dk Mlay, amesema hali za majeruhi wengine waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru, zinaendelea vizuri. Mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo, amewatembelea majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa mahospitalini. Viongozi mbalimbali wa CHADEMA wametembelea eneo la tukio.







From Chadema blog

0 comments: