Saturday, June 8, 2013

TWENDE TAIFA STARS TWENDE

Ikiwa yamebaki masaa machache ili kipenga kipulizwe kuashiria mwanzo wa mechi kati ya Taifa Stars na Morrocco. Stars inaingia dimbani kukichapa na Morrocco ikiwa na kumbukumbu ya kuichapa timu hiyo mabao 3 kwa 1.
benchi la ufundi la Stars linaundwa na Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi),Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja wa timu), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
Kila la kheri Stars. Mungu ibariki Tanzania! Mungu ibariki Stars!

0 comments: