Wednesday, June 5, 2013

MANGWEHA AANGWA RASMI DAR

Mamia ya watanzania wajitokeza katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam Leo kuuga mwili wa Marehemu Albert Mangwear aliefariki Dunia Mwezi siku ya Jumanne ya Tarehe 28 Mei huko South Africa na mwili wake kusafirishwa na kurudishwa Tanzania siku ya jana na kuagwa leo jijini Dar es salaam kabla ya kusafirishwa tena na kuelekea Morogoro kwa ajili ya Mazishi. Zoezi la kuaga mwili wa marehemu katika Viwanja vya Leaders limezua Utata kutokana na watu kugambania kutaka kwenda kutoa heshima za mwisho mpaka Polisi walipoingilia kati zoezi hilo kwa kuwasimamia Raia hao kufuata utaratibu ili zoezi liweze kwenda kama lilivyopangwa. Mwili wa Albert Mangwear kwa sasa upo njiani kuelekea mjini Morogoro kwa ajili ya mazishi ambayo yamepangwa kufanyika kesho huko huko Morogoro.

0 comments: